Na Mwandishi wetu

Sakata la Mchungaji Mosses Magembe kujitoa kwenye kanisa la TAG limezua taharuki hivi karibuni ambapo maoni mbalimbali mitandaoni yalileta sintofahamu , huku wengi wakingoja kusikia sababu hasa za mchungaji huyo machachari kuamua kujitioa katika kanisa hilo ambalo anadai amelitumikia kwa zaidi ya miaka 50.

Akizungumza katika clip inayosambaa mitandaoni mchungaji magehembe alisema ana sababu tatu za kuamua kujitioa katika kanisa hilo amablo amalitumikia kwa weledi na unyenyekevu wa hali ya juu, akifafanua kuwa mosi, ilikuwa ni kukubaliana kwa kutokukubaliana na hoja za Viongozi wake wanaomuandama kwa kile alichosema ni nia yake njema ya kujenga uhamsho katika kanisa la Kristo, hoja inayotafsiriwa tofauti na baadhi ya viongzi wa kanisa hilo kwamba ni kulinanga kwa matusi mazito kanisa la TAG.

“Mimi ninseme ukweli na mara zote nimekuwa Nikisema wazi kwamba kanisa limepotoka, limeangamia limepoteza misingi yake ni kama lipo ICU, na huu ni ukweli na nimekuwa Nikisema hivyo bila kuficha si kwa nia mbaya na sikulienga TAG peke yake nilimaanisha makanisa yote ulimwenguni yanaharibiwa na usasa kwa kuingiza vitu ambavyo ni kinyume na misingi ya Kristo,” alisema Magembe katika clip hiyo.

Aliongeza kuwa sababu nyingine kuu ilikuwa ni viongizi wake akiwemo Barnabas Mtokambali kutomuelewa na kumshutumu kwa hoja ya yeye kubariki mchungaji wa kanisa linguine, kiyu ambacho aliweka wazi kuwa hiyio si dhambi na si mara moja ni mara nyingi sana wachungaji wa kanisa ama madhehebu fulani kubariki wachngaji wa kanisa linguine.

“Mtoto wangu Yihana Magembe amabye kwa miaka kadhaa amekuwa msaidizi wangu wa karibu alipoanzisha huduma ya kiroho huko nchini Canada ilibidi nimbariki, nimuwekee wakfu, sioni kama hilo ni kos ahata kidogo, lakini wenzangu wamenishutumu kwamba nilichota mali za TAG kwenda kuanzisha kanisa linguine mahali fulani, hii ni upotishaji na si kweli,” alisema Magembe.

Aliongeza kuwa sababu ya tatu  ni yeye kuonekana amezeeka na asingependa kuzidi kukaamahali ambapo anawakwaza wengine na kuamua kuanzisha hudumamahali pengine, kitu ambacho anadai kingemfaa yeye na washirika wengine kusonga mbele na kuanzisha huduma anayohisi inawapeleka watu mbiguni.

“Kwasasa nipo Kinyerezi, karibu na ATN filling station, nimeanzisha huduma ya uhamsho, na wengi watadhani nilianzakujenga kwa muda mrefu ili niondoke TAG nikiwa nimejiandaa, la hasha, hapa mnaona hakuna sakafu, vijana wamezeka bati hili kwa usiku na mchana na leo tarehe 25 tumeanza huduma humu, mnaona kazi ya Mungu inasonga mbele,nsmshukuru sana muumini mmoja kajitolea bat izote hizi na kutoa sadaka najua hapombeleni tutafika pazuri, Mungu yupo na anajua dhamira yangu ya dhati,”alisema mchungaji huyo ambaye mara zote amekuwa akipinga nyimbo za maadhi ya ragge na soukousi katika kanisa la TAG, na hoja ya wanandoa kufunga pingu za maisha wakiwa tayari ni waja wazito.

Kwa upande wake mtoto wa mchungaji Magembe, Yohana Magembe alipnekana kuushutumu waziwazi Uongozi wa TAG akisema kuwa limekuwa na mambo ya kipuuzi na shutuma zsizo na kichwa na miguu dhidi ya baba yeke na kusema kuwa ameanzisha huduma nyingine nchini Candana na maeneo mengineinazidi kukuwa hukua akisema ni uzushi na uwongo kusema kuwa kuna mali za TAG Majumba Sita zimehamishwa kuanzisha kanisa lake.

“Niseme wazi kwamba mzee wangu umri umesonga anahitaji kuombewa na kutiwa moyo kwa kazi ,ubwa aliyoifanya badala ya kumdhihaki kwa hoja za kijinga. Mimi nimekuwa msaidizi wake wa karibu kwa miaka mingi na kanisaidia kukuwa kiroho, sasa anayekuja kumdhihaki pasipo kujua jinsi ushawishi wake ulivyotukuza sisi hadi tunaanzisha huduma nyingine lazima tumshangae sana. Baba hapaswi kuteseka kwa hoja za kijinga namna hii,” alisema mchungaji Yohana Magembe.

Kwa upanse wa makabidhiano rasmi ya kanisa hilo la Majumba Sita, Mchungaji Magemeb alisema kuwa alimuandaa mwanasheria wake ili kuweka mambo kisomi na kuongeza kuwa tayari amekabidhi gari aina ya landcruiser alilokuwa akitumia, muda wote, kakabidhi shule ya sekondari yenye mabweni na madarasa kadhaa pamoja na uwanja mkubwa wenye zaidi ya ekari tatu.

“Niseme wazi hapa ni mahali nilipopajenga kwa kipindi kirefu na nimemua kuachilia ilia mani ya moyo ibaki, siwezi kudhulumu mali ya kanisa mimi ni mwkweli, nimekabidhi mali hizi kupitia mwanasheria wangu, isipokuwa kuna mali zangu binafsi ambazo nilizileta mimi kamamimi imebidi niondoke nazo kuanzisha huduma mahali pengine. Zipo speakers am,bazo nimekuwa nikizunguka nazo muda wote, hizi na mali nyingine nimeondoka nazo,” alisema mchungaki megembe.

Kwa upande wake msaidizi wa Askofu mchungaji Magnusi Mpendakula Mhiche alizungumzia Sakata hilo na kufafanua kuwa kanisa la TAG halikumfukuza Magembe hata dakika moja na kuongeza kuwamtumishi huyo kaondoka kwa hiari, na mara zote amekuwa kaituhumiwa na kuitwa kwenye vikao kujibu shutuma anazotoa dhidi ya Viongozi wake pasipo kujirekebisha.

“Namheshimu sana huyu mzee amefanya kazi kubwa na tuliwahi kumpa nafasi makao makuu akiwa katibu wa missioni na uinjilisti, alifanya kazi znuri sikatai, lakini hoja ya kulishutyumu kanisa na kutudharau alkisema TAG iko ICU kweli tulisononeka na kushangaa kwamba basi kama tuko taabani kitanda hiki huenda mwenzetu naye kalala kitanda cha pili na askiofu mkuu yupo kitanda cha tatu, wote ICU,” alisema Mhiche na kuongeza kuwa pamoja na hayo amekuwa akihuzunishwa na namna ambavyo yeye Magembe amejipambanua kama mtakatifu aneyelipeleka kanisa kwenye unyoofu kupitia uhamsho huku maaskofu wakionekana ni wapotoshaji wa msingi ya kanisa.

“Niseme wazi kwamba tuna Askofu wetu Barnabas Mtokambali ni mvumilivu sana, kapokea mishale mingi kutoka kwa waamini wakimwambia inakuwaje babba Magembe anawashutumu hivi na hamchukui hatua…sasa tukaona tumvumilie mpaka yeye mwenyewe alipoona hapa kweli hapamstahili,” alisema Mchungaji Mhiche kwenye clip inayosambaa mitandaoni.

Mchiche aliongeza kuwa alipokea barua ya Mchungaji magehembe kutaka kujiondoa kwenye kanisa hilo mnamo tarehe 13 december, 2024,huku ikiwa na hoja za yeye kutokukubaliana na namna anavyotuhumiwa yeye na mwane kuanzisha huduma nyingie ikiwa ni pamoja na kumbariki mtoto wake kuanzisha kanisa mahali pengine.

Hata hivyo Mchungaji Mhiche aliongeza kuwa ni ukweli kwamba alipowahoji baadhi ya vongozi na wazee wakanisa la Majumba sita walikiri kufanyishwa harambee kuchangia huduma ya kanisa jipya la mtito wake, kitu alichosema ni kinyume na katiba pamoja na taratibu za kanisa hili, hyku akifafanua kuwa utaratibu ni kwamba mali za TAG na mcihango yote ilibidi ijenge kanisa hilio moja na sio vinginevyo.’

“Alitokea kijana mmmoja ni kama alipangwa kwenye mkutano wa majumuisho akasema anaaamini Magembe hapa hapamfai aanzishe huduma nyingine, akatutukana mimi na askofu kwenye kikao, tukashangaa alikotoka ni wapi, akasema yeye haoni kama kuna Uamsho kwenye hili kanisa analohudumu Magembe, mkamilifu ni Magembe na ilibidi ahame ili kuwabariki walio wengi,” alisema Mhiche, na kuongeza kuwa inapotokea vijana walioishi kwa sadaka kama alivyo mtoto wa Magembe na kuaza kutukana Viongozi wakubwa hii haileti afya hata kidogo.

Mhiche alifafanua kuwa anamtakia kila la heri mchungaji mMagembe huko aendako katika kumtumika Mungu kwa viwango vingine na kuwatahadharisha waamini kuwa ni kitu alichokipnga tangu mwaka 2014, kwani hata alipohamia anasikia tayari kukishakuwa na uwanja na wamejenga kanisa.

“Hii si kitu ya ghafla, mwenzetu alijipanga kuanzisha huduma…nawaomba hata manaotaka kumfuata muwe makini na mambo mawaili, misingi ya kanisa hilo jipya imesimama katika nini, pili angalisa leadership structure yake ikoje,” alisema Mhiche na kuongeza kuwa inapotokea kanisa lina Askofu amabye yeye nio mtunza hazina na ndiye katibu huku mkewe akiwa ndiye msaidizi wake, na mtoto wake ni msemaji mkuu, hapo hakuna misingi na ikitokea kama yaliyotupata sisi maana yake hakuna Kamati kuu inayowezakuamua bali ni maamuzi ya mtu mmoja tu. 

Mhiche alisema ni sharti misingi ya kanisa iangaliwe na Kulindwa huku akitamba kuwa pamoja nakuona kuna mali kadhaa mwenzao kaondoka nazo bado TAG itazidi kuwa imara, huku akifafanua kuwa wanao uwanja mkubwa na wana mpango wakuboresha jengo hili waamini wapte ventilation znuri na kuabudu mahali pazuri.

Kwasasa Kanisa na Majumba Sita litakuwa chini ya Mchungaji Mpya, Danstani kanemba, amabye atasimikwa rasmi na Uongozi mpya wa TAG makau makuu, iliikika sauti ya mtangazaji wa Ny TV, kwenye clip inayosambaa mitandaoni. 

Tanzania imekuwa na mogogoto mingi ya madhehebu ambapo hivi karibuni mchungaji wa Monique Dibwe raia wa DRC alionekana kuwaibia washarika kwa kuwataka wachangie Sh500,000 kwa kila mmoja anayetaka Maombezi, huku serikali ikiingilia kati kupinga ibada hizo na mahubiri chonganishi na kumtaka aondoke nchini. Na akiwa nchini kwao amekuwa akiwatukana Watanzania kwamba ni wajinga ndio waliwao na kuonesha magari ya kifahari ambayo aliyanunua kupitia fedha za waamini. 

Post a Comment

Mpya zaidi Nzee zaidi